Categories
About WFBG

Swahili

KIKUNDI CHA WAZUNGUMZAO LUGHA MBILI CHA WALTHAM FOREST(WALTHAM FOREST BILINGUAL GROUP) – KINACHOSAIDIA FAMILIA ZENYE KUZUNGUMZA LUGHA MBILI.

Kuzungumza zaidi ya lugha moja kunaleta faida nyingi – kwa watoto, kwa jamii yetu, kwa uchumi wetu. Lakini mara nyingi kutokana na ukosefu wa maelezo, wazee wenye kuzungumza zaidi ya lugha moja huchagua kuzungumza na watoto wao kwa lugha ya kingereza. Zaidi ya asilimia 20 ya watu wanaoishi Waltham Forest huzungumza lugha nyengine ambayo si lugha ya Kiingereza, lakini Uingereza inabakia kuwa ni nchi ya lugha moja, kwa sababu kuzungumza lugha moja inaonekana ni jambo linalokubalika, ingawaje ukweli wa mambo ni kwamba zaidi ya thuluthi mbili ya watu duniani wanazungumza lugha mbili. Kuzungumza lugha moja peke yake ni chaguo la mtu, sio jambo la kawaida.

Kikundi cha wazungumzao lugha mbili cha Waltham Forest -Waltham Forest Bilingual Group (WFBG) ni kikundi cha kujitolea cha wazee wenye lugha zaidi ya moja kilichoundwa mwaka 2003. Lengo letu ni kuchangia, kulea, kuhamasisha na kusherehekea tofauti za kiutamaduni na za kilugha kwa kusaidia wazazi kukuza watoto wao kwa kujua lugha mbili.

  • Mkutano wa kila mwezi kwa wazee na watoto: WFBG hukutana mara moja kwa mwezi siku ya jumamosi mchana sehemu iitwayo “Limes Children and Community Centre katika Walthamstow kutoka 3.30 – 5.30). Tafuta “Lime Centre” kwenye ramani
    Nafasi ya ya kuzungumza na wazee wengine wenye kuzungumza lugha mbili wakati watoto wanacheza! Limes ni kituo kizuri sana chenye vifaa vizuri vya kuchezea kwenye bustani , mipira ya vidibwi vya ndani ya nyumba na amali nyingi za mikono za watoto kujifunza. Wanachama wa WFBG wanaweza kuazima vitabu, kuchukuwa vitabu vilotolewa msaada, na vitu vengine katika lugha tofauti na kuzungumza na wazee wenye uzoefu zaidi kuhusu masikitiko au maswali yeyote watakayokuwa nayo. Watu wote wanakaribishwa, hapana haja ya kupiga simu kabla, unaweza kuja tu!Tafadhali angalia kalenda yetu kwa kipindi kinachofuatia.
  • Ujuzi wa utendaji darasani “Workshops” kwa wazee wapya: workshop itatumia mazoezi mepesi, mazungumzo, na vipindi vya maswali na majibu kutoa utangulizi mfupi kuelezea kile walichojifunza wanachama wa kikundi hicho kama vile nini linalofaa na katika familia gani? Workshop zetu inaendeshwa na wazee kwa wazee.
    *Hatua ya Kwanza *: Workshop kwa wazee wenye watoto kuanzia 0-3
    *Hatua Nyengine*: Workshop kwa wazee wenye watoto wenye miaka 4 na zaidi inayolenga kuendeleza lugha zaidi ya moja pale watoto wanapoanza kusoma na kuandika. Angalia kalenda yetu kwa tarehe na matukio maalumu.
  • Vipi unaweza kusaidia juhudi za WFBG: kwa miaka mingi iliopita,WFBG imetoa ushauri na msaada kwa mamia ya familia zenye kuzungumza lugha nyingi katika Waltham Forest na Kaskazini Magharibi ya London (North East London). Juhudi zetu zote ni bure kwa yule anayetaka kushughulika na mambo ya kuzungumza lugha zaidi ya moja (Ingawaje wale wanaohudhuria vipindi hivi kwa kawaida wanaalikwa kuchangia £12 kwa mwaka, £6 kwa familia zisizokuwa na kazi). Gharama zilobakia za huduma zetu, tunahitaji msaada kutoka kwa wadhamini na jumuia nyengine.
    Ukitaka kuwa ni mwanachama au kusaidia kikundi chetu tu, tafadhali wasiliana au hudhuria kwenye mkutano wetu unaofuatia hapo Limes.

MIONGOZO MUHIMU KWA WAZEE

  • Usipokee ushauri wowote wa kukufanya uache kuzungumza lugha yako kutoka kwa daktari, mwalimu, mkaguzi wa afya au mkunga. Omba uhamishiwe kwa mtaalamu wa matamshi anaezungumza lugha mbili atakaekupa muongozo wa hali yako kwa kina zaidi, inawezekana akakushauri ufanye kinyume na hao wengine. Kulikuwa na fikra kwamba kuzungumza zaidi ya lugha moja inawatatanisha watoto.Wazee mara nyingi bado wanafikiria ikiwa mtoto anazungumza lugha zaidi ya kingereza nyumbani, watafanya vibaya shuleni. Imani hizi zimeonekana kuwa hazina ukweli, utafiti unaonesha kwamba watoto wenye lugha zaidi ya moja waliozaliwa ungereza au waliofika hapa walipokuwa wadogo sana wanafanya vizuri shuleni na kwa uhakika zaidi hufanya vizuri zaidi kuwashinda watoto wenye kuzungumza lugha moja peke kwenye kazi zinazohitaji mawazo.
  • Zungumza lugha yako asili au lugha yako ulio na ufasaha nayo zaidi kwa watoto wako. Ingawaje ni hekima nzuri kuhakikisha watoto wako wana uwezo mzuri wa kingereza kabla ya kuanza shule kwenye umri wa miaka 4 au 5, mwisho wake kuna uwezekano zaidi kupoteza lugha yao ya pili ukilinganisha na kingereza hata kama hawatazungumzishwa kingereza wakati wapo wadogo. Watoto wadogo hukamata lugha ya kingereza kwa haraka sana kupitia viwanja vya michezo na nasari.
  • Tumia vifaa vyote katika lugha yako: TV, michezo, michezo – ya bao, DVD, vitabu, michezo ya computer na kutembelea jamaa na marafiki. Utakapoengeza juhudi zaidi katika lugha yoyote , kwa njia ya ubora na kwa wingi, utapata mafanikio zaidi katika lugha hiyo.
  • Jiwekee lengo na uamue vipi umuhimu wake kwako wewe. Unataka mtoto wako aweze kuzungumza na kufahamu peke yake? Unataka waweze kusoma gazeti, kuandika barua, kujipatia kazi?
  • Mwisho kabisa na muhimu zaidi, usikate tamaa. Watoto wengi wenye wazee wanozungumza lugha mbili, mwisho wake huishia na lugha moja, hutokezea hivi kwa sababu wazee wao wamekata tamaa. Kutakuwa na dhiki na baadae faraja. Watoto watakataa na kukuambia kwamba hawataki kuzungumza lugha yao iliyo dhaifu. Usiwalazimishe kuzungumza lugha yako, lakini wakati huo huo usikate tamaa kuzungumza nao kwa lugha yako. Endelea kumuonesha mtoto wako vipi umuhimu wa lugha kwako na hamu yako ya kuwa na uwezo wa kuitumia. Ingawaje watoto baadhi ya wakati huona tabu kuzungumza lugha yao ya asili, watu wazima wenye kuzungumza lugha mbili huwashukuru sana wazee wao kuwa wamejitahidi na hawakukata tamaa.

Kitabu cha Claire Thomas kilichochapishwa mwaka 2012 kiitwacho “Growing up with languages – Reflections on Multilingual Childhoods,” kilichotolewa na “Multilingual Matters”. Kitabu hiki kinalenga kwenye uzoefu wa watu waliokulia wakizungumza lugha mbili au zaidi na kinatoa muongozo katika nyanja tofauti za misingi kwa wanozungumza lugha mbili.

Kama unafikiri unaweza kusaidia kutafsiri kwa lugha yako, tafadhali wasiliana nasi.